Pages

Subscribe:

Friday, January 26, 2018

MR BLUE: NAJIWEKA MBALI NA WANAWAKE KAMA ALIKIBA

Rapper wa bongo Kherry Samir a.k.a Mr. Blue ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa 'mbwa koko' amefunguka na kudai sababu kubwa iliyompelekea kumtaja Alikiba katika ngoma hiyo ni kutaka kujiweka mbali na wanawake wanaoshindwa kujistili .

Mr. Blue amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya watu wengi kuuchukulia wimbo huo kama 'diss track' kwa wasanii ambao...
amewataja ndani ya ngoma hiyo na kusema alichofanya yeye ni majigambo na katika sanaa anayoifanya inamruhusu kufanya hivyo.

"Nimetaja wimbo wa 'seduce me' kwa sababu kuna 'line' zinazungumzia jinsi ya wakina mama wanavyoshindwa kujistili, kwa hiyo mimi lazima nigeuke kama Alikiba uni-seduce kwa sababu hutoniweza kukaa na mimi 'so seduce me like' Alikiba. Mimi sija-disi mtu katika nyimbo yangu ila nimezungumzia changamoto za upande wangu wa 'rap", alisema Mr. Blue.

0 comments:

Post a Comment