Pages

Subscribe:

Saturday, January 27, 2018

AUNT LULU ATOA OFA YA PENZI KWA PAPII KOCHA KISA MWONEKANO


Mwanadada aliyewahi kuwa mtangazaji ambaye haishiwi na matukio, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ amesema kuwa yupo tayari kumpa ofa ya mapenzi mwanamuziki Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ mpaka asahau maisha aliyopitia.

Akiongea Aunt Lulu alisema amemuona Papii amekuwa mpya na anapendeza kila kukicha hivyo amejitolea kumpatia penzi iwapo atamkubalia ili...
asahau kabisa shida za dunia.

“Unajua mimi najua kupenda, iwapo nitampatia penzi Papii mbona atasahau kabisa alipotoka, yeye akubali tu maana sijawahi kuona mahusiano yake, naamini kwa kipindi alichokaa jela kama angekuwepo mwanamke angejitokeza lakini haijawa hivyo, mimi nipo kwa ajili yake,” alisema Lulu.

Mwandishi wetu alijaribu kumpigia simu Papii ili kumfahamisha juu ya ofa hiyo ya mapenzi lakini hakuweza kupatikana mara moja.

Source: Global publishers

0 comments:

Post a Comment