Pages

Subscribe:

Tuesday, January 30, 2018

HIVI NDIVYO ARSENAL INAVYOMTESA MADEE

Pamoja na ripoti za leo kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari barani Ulaya kueleza kuwa nyota wa Borussia Dortmund na Gabon Pierre Aubameyang anakaribia kujiunga na Arsenal msanii, Madee bado hana imani. 

Nyota huyo wa HipHop anayetamba na ngoma ya 'Nanii' aliyoshirikishwa na msanii wake anayeitwa Gaza ameiambia East Africa Television kuwa, huwa hana imani na tetesi za usajili wa klabu hiyo anayoishabikia mpaka...
pale atakapoona mchezaji anatambulishwa rasmi.

''Tetesi zimekuwa nyingi sana na kwangu ninavyoifahamu timu yangu mpaka nione mchezaji amevaa jezi yetu ndio naweza kuamini, kwasasa siwezi hata kuposti chochote kuhusu Aubameyang'', amesema.
Mapema leo imeripotiwa kuwa Arsenal na Dortmund zimekubaliana baadhi ya vipengele kwaajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2015 kutua Arsenal kwa dau la £ 60m takribani shilingi bilioni 167.

0 comments:

Post a Comment