Pages

Subscribe:

Sunday, January 28, 2018

BINTI AJIUA BAADA YA KUTUMA SMS KIMAKOSA KWENDA KWA MPENZI WAKE

Msichana wa miaka 17 Charlotte Guy ambaye ni mwanafunzi wa chuo nchini Uingereza hivi karibuni amekutwa amejinyonga baada ya kumtumia mpenzi wake meseji kwa bahati mbaya aliyotaka aitume kwa rafiki yake ya kumwambia kuwa amelala na mwanaume mwingine.

Inaelezwa kuwa Charlotte alituma meseji hiyo kwa mpenzi wake huyo Jack Hurst mwenye miaka 20 ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo kingine, akiwa anataka kumwelezea rafiki yake jinsi...
alivyolala na mwanaume huyo usiku wa jana yake waliokuwa wametoka.

Baada ya kugundua alichokifanya alimtumia Jack meseji tatu mfululizo zisemazo "Kwaheri. Tafadhali nisamehe, Nakupenda, kujua kwamba unanichukia inatosha."

Jack ameeleza polisi kuwa baada ya kupokea meseji ya kwanza ya mpenzi wake kulala na mwanaume mwingine, mpenzi wake huyo alijaribu kumpigia lakini alimwambia hajisikii kuongea wala kujibu meseji na baada ya muda mfupi ndipo alipoona meseji hizo za kumuaga.

Wazazi wa Charlotte wameeleza kuwa binti yao amewahi kujaribu kujiua na amekwisha wahi kusikika akizungumza kuwa anaweza kujiua.

0 comments:

Post a Comment