Pages

Subscribe:

Saturday, January 27, 2018

MAHER AL BARUAN KUZUNGUKA NCHI 47 ZA AFRIKA KWA PIKIPIKI

Aamua Kuizunguka Afrika Nzima kwa Kutumia Pikipiki
Mwendesha Pikipiki kutoka Uarabuni ameamua kuizunguka Afrika nzima anakusudia kufanya ziara yake katika nchi 47, akianzia safari yake nchini Oman.
Maher Al Baruan amepania kuweka historia ya kuwa raia wa kwanza wa Oman kuizunguka Afrika akitokea kwenda kusini kupitia mashariki kisha atapanda Oman kupitia...

Magharibi mwa Afrika.
Safari yake ilianzia nchini Oman mnamo mwezi wa saba mwaka 2017.

Mpaka sasa amekwisha safiri kwa miezi 7 na anasema safari yake itachukua zaidi ya mwaka kuikamilisha.

Wahenga wanasema, msafiri kafiri na mwenda pole hajikwai.

Lakini je, amejifunza nini katika safari yake? Akiwa mjini Bujumbura Maher Al Baruan ameelezea mambo matatu ambayo amejifunza kuhusu Afrika.

1. Usalama

Changomoto kubwa Maher Al Baruan anasema anajihisi yuko katika hali ya hatari anaposafiri kwa sababu hajui atakutana na nani.

Anasema hata wanyama pori huwa ni jambo la kujitahadharisha.

Hata hivyo, anaelezea kuwa hajawahi kupata kisa chochote cha kumdhuru.

2. Umakini wa sheria za barabarani

'Nataka niirudie enzi za babu zangu' Maher Al Baruan
Maher Al Baruan amegundua kwamba waendesha pikipiki wengi ambao amewaona hawatilii maanani sheria za barabarani na hasa za usalama kwa kuvaa kofia ngumu.

'Ningewashauri waendesha pikipiki wafuate sheria za barabarani, wasivue kofia ngumu kwa sababu hizi zote ni kwa ajili ya usalama wao' ameelezea Maher Al Baruan.

Polisi watumia nyimbo kukabili ajali za pikipiki Tanzania
Ujumbe wa mfalme wa Oman wawasili Zanzibar
Uingereza: Muendesha pikipiki jela miezi 8 baada ya kujipiga selfie barabarani


3. Oman inapendwa
Maher anasema kuwa katika safari yake anakaa siku 35 kwa kila nchi anayoifikia ili kufahamu zaidi namna ambavyo watu wanavyoishi katika nchi hizo pamoja na kujua tamadani na kupata vionjo vya chakula.

Maher anataka kurudisha zama za babu zake wa Oman waliokuwa wakisafiri kanda ya Afrika Mashariki.

"Kila mmoja akishajua kwamba natoka Oman, wanaipenda nchi ya Oman na wanaiheshimu," anaelezea Maher Al Baruan.

0 comments:

Post a Comment