Pages

Subscribe:

Friday, January 26, 2018

MAUZO YA MONEY MONDAYS YAMCHANGANYA VANESSA MDEE



Msanii wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee  a.k.a V Money amezungumzia mapokezi  ya album yake ya ‘Moneymondays’ iliyotoka Januari 15 kuwa ni mazuri zaidi ya vile alivyotarajia.

akizungumza na Dizzim Online mkali huyo wa ngoma ya Kisela ambaye kwasasa amerudiana na mpenzi wake wa muda mrefu msanii Juma Jux amesema kuwa mauzo yako...
vizuri sana kuliko alivyodhani kwani Mashabiki na Wasanii wenzie wameonyesha kumpa nguvu sana katika Album yake.

“kiukweli namshukuru Mungu mauzo yanaenda vizuri sana  album imepokelewa vizuri  na tunazidi kupromote  amna kitu kikubwa zaidi ya kupromote na kupata nafasi ya kuisambaza sehemu mbali mbali so kiukweli tunatumia nguvu nyingi sana kuwashirikisha wakala wengi pande zote za Tanzania na pia tunampango wa kufika lagos, Mexico alafu pia tutaenda kigali kote ni katika kuisambaza album yangu”. amesisitiza Msanii huyo.

Vanessa Mdee ambaye alizindua App yake amesema kuwa Mashabiki wake waendelee kumpa Support hasa Mwaka 2018 kwani amewaandalia vitu vingi sana ambavyo vitaendelea kuupeleka muziki wa Bongo Fleva mbali zaidi.

0 comments:

Post a Comment