Pages

Subscribe:

Sunday, January 28, 2018

DIAMOND NA VANESSA WAPAMBANISHWA KUWANIA TUZO MOJA NCHINI NIGERIA

Leo January 27,2018 staa wa muziki Diamond Platnumz pamoja na Vanessa Mdee wamechaguliwa kwa mara nyingine tena kuwania tuzo za nchini Nigeria “Too Exclusive Awards 2017″ wote wametajwa katika kipengele kimoja cha msanii bora wa mwaka katika tuzo hizo zitakazofanyika nchini Nigeria.

Diamond na Vanessa Mdee katika kipengele hicho cha msanii bora wa mwaka, wote wanashindania tuzo hiyo na wasanii wengine kama...
Nasty C ( Afrika Kusini), Sauti Sol( Kenya), Sarkodie(Ghana), Cassper Nyovest(Afrika Kusini).



Kwa mujibu wa waandaji wa tuzo hizo wametaja kuwa kipengele hicho wanachowania wasanii Diamond Platnumz na Vanessa Mdee na wasanii wengine wengi, wameteuliwa wasanii mbalimbali lakini akihusishi wasanii kutokea nchini Nigeria. 

Taarifa hizo zinakuja ikiwa ni wiki mbili zimepita toka Diamond Platnumz ashinde tuzo ya Sound City Nigeria lakini ni tuzo ambazo Vanessa nae alikuwa anawania lakini hakubahatika kushinda, unaweza kuwapigia kura Diamond na Vanessa kupitia tooxclusive.com

0 comments:

Post a Comment