Pages

Subscribe:

Monday, January 29, 2018

ARSENAL WAKUBALI KULIPA PAUND MIL 55.4 YA PIERRE AUBAMEYANG



Klabu ya Arsenal imekubali kulipa kitita cha paundi milioni 55.4 kwa timu ya Borussia Dortmund ili kupata saini ya straika wao, Pierre-Emerick Aubameyang dili ambalo linaweka rekodi ndani ya timu hiyo kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa kiwango kikubwa cha fedha.

Arsenal imempatia, Aubameyang mkataba wa miaka mitatu na nusu ambao atakuwa akilipwa paundi 180,000 kwa wiki wakati timu hiyo ikiwa katika harakati za...
kuimarisha eneo lake la ushambuliaji.

Pierre-Emerick Aubameyang akitarajiwa kutua Arsenal kwa uhamisho wa paundi milioni 55.4

Mtandao wa, Sport Bild umeripoti kuwa klabu ya Borussia Dortmund imeamua kumchukua straika wa Chelsea, Michy Batshuayi kuziba pengo la Aubameyang.

Dortmund ilihitaji kumsajili Giroud laki uhamisho wa Mfaransa huyo ulikwama baada ya kufuatia familia yake kumuhitaji kusalia England.

Kutua kwa Aubameyang ndani ya Arsenal kunatoa tafsiri kwa Giroud kuelekea Chelsea kwa dau la paundi milioni 35 baada ya mazungumzo ya liyofanywa na timu hiyo mwishoni mwa juma.

0 comments:

Post a Comment