Pages

Subscribe:

Saturday, January 27, 2018

AFYA: HAYA NDIYO MARADHI 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YA NYUKI

Image result for HONEY
Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote.Vitabu vingi vya zamani vinazungumzia namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kutokana na asali. Moja ya vitabu hivyo ni KURUANI TUKUFU ambayo Mwenyezi Mungu 

anaitaja asali kama tiba(AN-NAHL 16:68-69). Sasa hivi kuna makala nyingi zilizo andikwa zikielezea kuhusu uwezo wa asali katika tiba ya magonjwa mbalimbali. Warusi na Wafaransa wanafahamika sana katika... kufanya utafiti katika maabara kuhusu uwezo wa asali katika tiba mbali na Kuruani Tukufu kuna.

baadhi ya vitabu vingine vinavyofahamika kuandikwa na watafiti kuhusu uwezo wa asali katika tiba. Moja kile cha BEES DON'T GET ARTHRITIS CHA FRED MALONE NA BEE IN BALANCE CHA AMBER ROSE.

Leo tuangalie tiba ya asali na mdalasini na namna ya kuitumia kutibu maradhi mbalimbali(asali tunayoizungumzia hapa ni asali safi mbichi.)

BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA KWA ASALI NA MDALASINI NI KAMA IFUATAVYO:

1.UGONJWA WA VIUNGO/MAUMIVU NA UVIMBE(ARTHRITIS)
-Chukua maji kiasi vuguvugu na ongeza mdalasini (unga kijiko cha chai na asali vijiko 2 vya chakula na kuchua sehemu zenye maumivu)
-Vilevile waweza kutengeneza kikombe kimoja cha chai kwa kuweka kijiko kimoja cha unga wa mdalasini na kuongeza asali vijiko viwili vya chakula na kisha kunywa ikiwa ya moto kutwa mara mbili(asubuhi na jioni)

2.KUKATIKA KWA NYWELE(HAIR LOSS)
-Asali ikichanganywa na mdalasini na mafuta vuguvugu ya olive hutia kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele.
-Tumia mchanganyiko huo vuguvugu kwa kupaka na kusugua kichwani na acha kwa dk 15 kisha uoshe.

3.UKUNGU WA MIGUU(FUNGUS)
-Changanya kijiko cha chakula cha asali na vijiko viwili vya chai vya mdalasini na acha kwa muda wa nusu saa kisha safisha .(rudia hivyo mpaka upone)

4.MAAMBUKIZI KWENYE KIBOFU CHA MKOJO(BLADDER INFECTION)
-Changanya maggy ya maji vuguvugu na vijiko2 vya chai vya mdalasini na kijiko1 cha asali huondoa bakteria kwenye kibofu.

5.MAUMIVU YA JINO(TOOTHACHE)
-Changanya sehemu tano za asali na sehemu moja ya mdalasini na dondoshea kwenye jino linalouma hadi maumivu yatakapotoweka.

6.VIDONDA VITOKANAVYO NA MAGONJWA YA KULALA KWA MUDA MREFU(BED SORES)
-Paka saladi iliyochanganywa asali na mdalasini.Vilevile tumia chai ya roseberry nyekundu kwa kuondoa maumivu makali ya canker sores/bed sores.

7.LEHEMU(CHOLESTRAL)
-Changanya asali safi mbichi vijiko2 vya chakula na unga wa mdalasini vijiko2 vya chakula na kikombe cha chai cha maji ya moto na unywe kutwa mara 3

8.MAFUA(COLDS)
-Tumia mchanganyiko wa kijiko 1 cha chakula cha asali vuguvgugu na robo kijiko cha unga wa mdalasini kuondoa chafya na kuvimba koo.

9.UGUMBA(INFERTILITY)
-Asali inaaminika kuamsha hamu ya mapenzi. Kwa wapenzi. wa jinsia zote wanashauriwa kunywa walau vijiko 2 vya chakula kila siku kabla ya muda wa kulala. Mdalasini imetumika muda mrefu katika dawa za kichina na kihindi kuongeza uwezo wa uzazi kwa akina mama wenye kuhitaji kuzaa.
 
-Changanya mdalasini na kiasi cha asali na kufanya mgando (paste)na upake kwenye fizi na meno na kuacha inyonywe na kuingia mwilini taratibu na hii ni kwa akina mama wasio na sababu za kimsingi za kuwakosesha kuzaa.

10.MCHAFUKO WA TUMBO(STOMACH UPSET)
-Asali kwa muda mrefu imetambulika kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko wa tumbo na kichefuchefu. Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali pia hupunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.

11.GESI(ACID)
-Kula asali pamoja na mdalasini kuondoa mchafuko wa tumbo na utumbo uletwao na gesi(acid)huu ni uchunguzi ulio fanywa na Japan na India

12.UGONJWA WA MOYO(HEART DISEASE)
-Unaweza kukinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara kwa kupakaa kama jam wakati wa kula mkate wa ngano wenye nyuzinyuzi nyingi iliyopakwa kijiko 1 cha chakula cha mchanganyiko huo(asali na mdalasini) kila siku

13.SHINIKIZO LA DAMU(H/B/P)
-Shinikizo la damu pamoja na matatizo yaambatanayo na maumivu ya kifua na kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya upata dozi ya mara kwa mara ya asali iliyochanganywa na mdalasini.

14.KINGA YA MWILI(IMMUNE SYSTEM)
-Kinga yako ya mwili itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini kwa pamoja.Utafiti unaonyesha kuwa hazina  kubwa ya vitamini(virutubisho),madini pamoja na mchanganyiko wa mdalasini na asali iondoayo magonjwa na kinga itolewayo na chembechembe nyeupe za damu husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea(virus)na bakteria.

15.UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME(UHANITHI/IMPOTENCE)
-Asali ina historia ndefu ya kuamsha nguvu ya uume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi kutokana na uwezo wake kama kiamshaji/chaji. Asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za mashariki za dunia.
 
Watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba asali inauwezo wa kupelekea mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo mdalasini.
 
-Katika Afrika na dunia ya kusini mabaharia wamekuwa wakipaka asali katika sehemu zao za nje ya uume ili kuongeza nguvu ya kufanya mapenzi.

16.KUTOKUCHAGULIWA KWA CHAKULA(INDIGESTION)
-Kula vijiko 2 vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo huondoa kiungulia na wataalam wanasema asali husaidia kutolewa kwa juisi zinazotumika kuchaguliwa kwa chakula tumboni na mdalasini unaongeza kasi ya kuchaguliwa kwa chakula.

17.FLU(INFLUENZA)
-Tafiti  moja ya Kihispania imethibitisha kwamba aina ya dawa iliyopo katika asali ni dawa moja asilia ya ajabu ambayo huharibu vimelea(virus)waletao flu.

18.KUONGEZA UMRI WA KUISHI(LONGEVITY)
-Unaweza kuishi hadi miaka 100 na kufurahia maisha ya afya na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai ya mdalasini na asali.Kutengeneza kinywaji hiki kitamu weka vijiko 
4(vikubwa)vya mdalasini na vijiko 4 vya asali,vikombe 3 vya maji na koroga kwa dk 10 kisha kunywa robo kikombe mara 3 au 4 na hivyo utakuwa na kinywaji kingi.

19.KUONDOA CHUNUSI(PIMPLES)
-Changanya vijiko 3 vikubwa vya asali na kijiko 1 kikubwa cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi.Uwezo wa asali wa kuua bakteria unafanya uso kuwa wa kawaida katika muda wa wiki 2.

20.KUUMWA NA WADUDU(WASHA WASHA WENYE SUMU)
-Changanya asali na mdalasini kisha pakaa moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia tena hadi uvimbe uishe.

21.MADHARA YA NGOZI(INFECTIONS)
-Fanya kama ilivyoandikwa namba ishirini hapo juu.

22.KUPUNGUZA UZITO.
-Waweza kufurahia vyakula vyote unavyovipenda kuwa na afya nzuri na kupunguza uzito wa mwili ambao hauhitajiki kwa kula chakula chenye nguvu na ladha nzuri kilichojaa vitu muhimu viwili ambavyo ni asali na mdalasini.
-Unachohitajika kufanya ni kuhakikisha unavitumia vyote kwa kiasi katika mapishi yako.Vilevile wataalam wanasema unaweza kuondoa mabonge ya uvimbe wa nyama nyama nje ya mwili kwa kuanza siku yako kwa kutumia vijiko 2 vikubwa vya asali na kijiko 1 cha mdalasini.Rudia mchanganyiko huo kabla ya kulala.Wataalam wamethibitisha kuwa inapunguza hamu ya kula na kuleta joto mwilini.

23.SARATANI(CANCER)
-Utafiti uliofanyika huko Australia na Japan umeonyesha kuwa asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya magonjwa kwa anaetumia madawa ya kutibu saratani.Katika tafiti iliyofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua saratani ya mifupa na utumbo ambao walikuwa wanatumia kila siku dozi ya asali na mdalasini walionyesha kupata nafuu maradufu kuliko wale waliokuwa wanatumia madawa ya kutibu saratani peke yake.Dr.HIROKI OWATA alisema waliwapa mchanganyiko wa asali na mdalasini kijiko kimoja kutwa mara 3 kwa mwezi 1 na wengine waliendelea kama kawaida.

24.KUONDOA UCHOVU(FATIQUE)
-Uko ushahidi kwamba sukari asilia iliyopo katika asali inauwezo wa kuongeza nishati mwilini.Zikitumika ipasavyo sukari hii inaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu.Wataalam wanapendekeza kuchanganya nusu kijiko cha asali katika nusu kikombe cha maji yaliyonyunyiziwa mdalasini kunywewa masaa mawili baada ya kuamka.Rudia kunywa saa 9 alasiri wakati nishati(nguvu)inapoanza kuisha kufuatia ushauri wa dr.MILSTON ABBOZZA ambaye kazi zake kuhusu asali na mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa.

25.KUVIMBA NYAYO(SOREFEET
-Changanya asali na mdalasini katika maji vuguvugu na uchue miguu(nyayo)zilizoathirika baada ya siku ndefu ya kazi au baada ya mazoezi marefu.Rudia kila asubuhi na unawe nyayo kwa maji baridi na vaa viatu.
 
26.HARUFU MBAYA MDOMONI
-Chukua maji ya vuguvugu changanya na asali na mdalasini kisha sukutua kila asubuhi.Katia Asia ya kusini mashariki watu hula kijiko cha asali na mdalasini ili kuondoa harufu mbaya(halitosis).Wataalam wanaamini uwezo wa kuua bakteria uliopo kwenye asali ndio unaopigana na harufu mbaya toka mdomoni.

27.KUPUNGUA KWA USIKIVU(LOSS OF HEARING
-Dozi za kila siku za asali na mdalasini hufanya hali ya usikivu kuwa makini kama ilivyogunduliwa na Wagiriki zamani.
-Kutumia mdalasini na asali kutakufanya uonekane kuwa na afya nzuri.

0 comments:

Post a Comment