Pages

Subscribe:

Saturday, January 27, 2018

HISTORIA NYINGINE KUWEKWA SIKU YA KESHO KATIKA MUZIKI WA MAREKANI



Usiku wa kesho ni wa kihistoria kwenye tasnia ya muziki duniani ambapo jijini New York, Marekani kwenye Ukumbi wa Madison Square Garden patawaka moto katika tamasha la ugawaji wa Tuzo za Grammy.

Tuzo hizo zitafanyika jijini hapo ikiwa imepita miaka kumi na tano tangu zifanyikie na muda mwingi zilikuwa zinachukua nafasi katika Jimbo la Los Angeles kutokana na...
gharama za uendeshaji.

Neil Portnow ambaye ni miongoni mwa waandaaji alisema gharama za kuendesha shughuli hiyo imekosti zaidi ya dola milioni 6 mpaka 8 ambapo mastaa mbalimbali watahudhuria.

Miongoni mwa mavazi yanayotajwa kupendezesha usiku huo ni tisheti nyeupe zenye ua rose ambazo watavaa baadhi ya mastaa wakiongozwa na Rita Ora, Justin Timberlake, Rapsody na wengine wengi waliojiunga kwenye kampeni iitwayo Times Up ya kusapoti usawa na haki kwa wanawake katika maeneo ya kazi.

0 comments:

Post a Comment