Pages

Subscribe:

Tuesday, April 28, 2015

BABBI AMSHIRIKISHA KIDUMU KWENYE WIMBO WAKE MPYA


Baada ya kutamba na nyimbo kadhaa alizofanya pekee yake bila kushirikikiana na mtu, Msanii Babbi sasa kamua kufanya nyimbo na Kidumu uitwao Hoi na amesema anauachia rasmi ijumaa hii ya May 1.
Babii anasema kuwa anaamini wimbo huu mpya wa Hoi aliomshirikisha msanii Kidumu utapendwa sana na watu maana ni...
wimbo aliojipanga vizuri sana katika kuundaa.
“ Namkubali sana Kidumu na ndio maana nikaamua kufanya naye wimbo huu, na jamaa kaonesha uwezo wake mkubwa sana katika kuimba humu ndani, kwahiyo sauti yake ilipokutana na yangu imefanya kitu kizuri sana, hivyo napenda kuwaambia mashabiki wangu wakae mkao wa kula maana hili ni bonge la nyimbo "
Babbi ambaye asili yake ni Mtanzania na Mburundi ila kwa sasa makazi yake yako nchini Marekani amesema alitaka kuonesha uwezo wake pekee yake kwanza kabla hajamshirikisha msanii mwingine mkubwa.
“Nimetoa video zake nyingi tayari na mtu akitembelea kwenye you tube yangu anaweza kuziona nyingi , na unajua ni vizuri kuonesha uwezo wako kabla hujamshirikisha msanii mkubwa”
Wimbo huo mpya wa Babbi uitwao hoi anaamini ni wimbo mkali sana na anasema ataachia kwamba audio kabla ya kutoa video ya wimbo huo

0 comments:

Post a Comment