Pages

Subscribe:

Tuesday, April 28, 2015

JOKATE AGEUKA TAPELI ASAKWA USIKU NA MCHANA

Wakati akiwa na mkataba wa shilingi bilioni nane na nusu wa bidhaa zenye nembo yake kutoka Kampuni ya Rainbow Shell Craft, mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amekwaa kashfa ya utapeli akidaiwa ‘kuchikichia’ shilingi...
elfu sabini za msanii wa Bongo Fleva anayefahamika kwa jina la Abdallah Hamis ‘Planet’, 
Msanii wa Bongo Fleva, Abdallah Hamis ‘Planet’ akibisha hodi kwenye geti la Jokate bila mafanikio.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Planet alimuomba Jokate ashiriki kama ‘video queen’ kwenye video yake iitwayo Jokate ambapo walipatana kazi hiyo kwa shilingi laki moja na nusu ndipo Planet alipotanguliza kianzio cha shilingi elfu sabini.
“Baada ya makubaliano ya mdomo, Planet alimkabidhi Jokate shilingi elfu sabini kama advance (kianzio) ili atakapomaliza kazi, ammalizie shilingi elfu themanini iliyobaki

Planet aliyetapeliwa pesa na Jokate.

. “Sasa cha kushangaza, siku waliyopanga kufanya kazi, Jokate hakutokea katika eneo walilokubaliana na hata alipopigiwa simu hakupokea tena ndipo Planet alipoanza kumsaka kila kona bila mafanikio,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya chanzo hicho kumwaga ubuyu huo kwenye meza ya Ijumaa Wikienda, mapaparazi wetu walimvutia waya Planet ambapo alidai kuwa anashindwa kumuelewa Jokate kwa kitendo chake cha kumuingiza mjini.
“Dah! Unajua ile ngoma yangu nimemuimba yeye kwa lengo zuri tu kwa kuwa mimi ni shabiki wake, sasa baada ya kuachia audio nilipofikiria suala la video nikaona bora nimshirikishe awe video queen nikiamini itapendeza zaidi kwa kuwa itakuwa imeonesha uhalisia, nilimwambia akakubali baada ya kuisikiliza na kuipenda.
“Mchakato huo ulikuwa tangu mwaka jana mwezi wa tisa na makubaliano yetu alitaka nimpe laki moja na nusu, lakini akaniambia nimpe kianzio shilingi elfu sabini, cha kustajabisha tangu hapo amekuwa akinichenga hata nikipiga simu hapokei pamoja na kwenda nyumbani kwao mara kadhaa kumuulizia lakini huwa haoneshi hata kutaka kunisikiliza natimuliwa na walinzi,” alisema Planet huku akirekodiwa sauti.

Ili kutaka kuwaridhisha wanahabari wetu, Planet aliwaomba waende naye nyumbani kwa Jokate, Oysterbay jijini Dar  kushuhudia namna ambavyo amekuwa akipigwa chenga kila anapodai chake.

Mapaparazi wetu walipofika nyumbani hapo huku wakipiga picha hatua kwa hatua, walishuhudia Planet ‘akichomeshwa mahindi’ bila geti kufunguliwa licha ya kugonga kwa muda mrefu

Wakati Planet akiwa getini hapo, Jokate aliwasili akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Carina ambapo alishusha kioo na kumwambia msanii huyo kuwa yupo bize amtafute kwa simu.

Baada ya kumwambia maneno hayo, Jokate aliingia ndani kisha walinzi kufunga geti na kumwacha Planet akiwa nje.
JOKATE ANASEMAJE?
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Jokate kwa njia ya simu ambapo alipopatikana alijibu kwa kifupi kuwa hamfahamu Planet na kwamba anatafuta umaarufu kupitia jina lake.
“Simfahamu huyo msanii labda anatafuta kiki tu.”


0 comments:

Post a Comment