Pages

Subscribe:

Wednesday, April 22, 2015

DIAMOND AGUSWA NA KILIO CHA WEMA SEPETU

Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameeleza kulifahamu kwa muda mrefu tatizo la aliyekuwa mpenzi wake , Wema Sepetu la kutoshika mimba. Akiongea na kipindi cha Ng’ari Ng’ari cha Clouds TV, Diamond alisema wakati wako pamoja waliwahi kuzunguka kwa wataalam mbalimbali kujaribu kupata tiba lakini hawakufanikiwa. Alisema ilifika wakati alimweleza tu kuwa akubali hali hiyo. 

Diamond alizungumzia pia lile andiko la Wema Sepetu mtandaoni ambapo alielezea tatizo Akizungumzia andiko la Wema mtandaoni juu ya tatizo lake la kutoweza kupata mtoto, Diamond alisema aliumizwa na andiko hilo kama...
wengine walivyoumia, na alimsifu kwa kuusema ukweli japo hakufyrahishwa na watu walivyomshambulia kwa komenti za maudhi kwani anaumia kama  binadamu wengine.

0 comments:

Post a Comment