Pages

Subscribe:

Friday, June 26, 2015

OMMY DIMPOZ AMPA SIFA MENEJA WAKE

Star anaetamba na Single ya wanjera(Ommy Dimpoz) amesema mafanikio yake ya kimuziki yametokana na usimamizi mzuri anaoupata toka kwa meneja wake(Mobenga). Akiongea na E-News ya EATV Ommy Dimpoz ameongea mambo mengi yahusuyo muziki wake na pia ameongea kuhusu umuhimu wa meneja katika muziki wake kwa ujumla. Ommy Dimpoz amesema: "Wakati naamua kufanya kazi kama Solo Artist kulikuwa na umuhimu wa kuwa na meneja maana mwanzo kuna changamoto nilikuwa napata kama... kufuatilia kazi zangu mwenyewe n.k, Pia nilikuwa na wakati mgumu sana kipindi hicho sababu nilikuwa sina hata usafiri na nilikuwa napanda daladala, foleni zilikuwa zinafanya nichelewe mazoezini, Nilipoamua kuwa Solo Artist nilimtafuta Mobenga nikaongea nae na nikatoa wimbo wa "Nai Nai".

0 comments:

Post a Comment