Pages

Subscribe:

Friday, June 26, 2015

WOLPER: MIMI NI FREE MASON TANGU KITAMBO TU

Mtoto mzuri katika tasnia ya uigizaji Bongo, Jacqueline Wolper Massawe ‘Twiga wa Jangwani’ amesema haoni sababu ya kuukana uanachama wa taasisi ya Wajenzi Huru (Freemason) kwani ni dini kama zilivyo zingine na kama katiba inavyoelekeza, kila mtu anayo haki ya kujiunga na dini au taasisi yoyote ya kuabudu kulingana na matakwa ya imani yake...
Akiongea na mwandishi, Wolper alisema ni kweli yuko katika kundi hilo huku akishangaa watu kustaajabu kuona mtu yuko Freemason wakati walioanzisha dini hiyo ni binadamu kama wengine.

“Freemason si ni taasisi au dini kama zingine? Kuna ajabu gani mimi kuwa mwanachama? Tena nataka nikuhahakikishie kuwa, nimekuwa muumini halisi wa Freemason kwa muda mrefu sasa,” alisema Wolper.

0 comments:

Post a Comment