Pages

Subscribe:

Wednesday, June 24, 2015

BELLE 9:VIDEO ZA KIBONGO ZINAFANANA ILA YANGU ITAKUWA TOFAUTI

Belle 9 anatarajia kufanya video ya "Shauri zao" ambapo kasema anatarajia kuja na kitu tofauti kutokana na mfanano wa Video nyingi za Kibongo. Akizungumza katika kipindi cha E- News cha EATV, Belle 9 amesema: "Unajua sasa hivi video nyingi ukiangalia zinafanana location. Siwezi kuzitaja hizo video, sikupenda sasa hivi video itoke kwa kuwa sitaki... ifanane na zingine ndio maana tunatumia muda mrefu kutafuta location ili iwe tofauti na video zingine na iwe video ambayo inaendana na wimbo. Kazi zangu mashabiki wanazijua na kila ngoma inayotoka huwa kali zaidi ya ile na sidhani kama kuna Msanii anaweza kuwa hivyo kama mimi.

0 comments:

Post a Comment