Pages

Subscribe:

Wednesday, July 22, 2015

DIAMOND PLATNUMZ ADAI KUWA JOKATE NI MNAFIKI

Diamond Platnumz Akiojiwa na Clouds FM kuhusu Video aliyopost jana ikionyesha Jokate Akicheza Wimbo wake na Kuandika "Mbona Bado, Mtanyooka tu".Amesema kuwa yeye amempost kwa nia nzuri tu na si kumzalilisha amedai yeye mara nyingi huwa anawapost watu wakicheza nyimbo zake hivyo kumpost Jokate kwake ni Kawaida...
Pia ameulizwa kuhusu maneno aliyotumia kwenye video hiyo kuwa ni ya kichokozi Diamond akadai kuwa yeye ni Mswahili wa Tandele kuandika Maneno haya ni kawaida kwake kwani amekuwa akiyatumia katika post zake mbali mbali....lakini leo ametumia kwa Jokate basi watu wengine wamepanic.....

Mwisho Diamond Akafunguka ya Moyoni kuhusu Jokate na Kusema kuwa si mzalendo kwa vile anajidai kumpongeza leo baada ya kushinda wakati kabla ya kushinda yeye na wenzake walikuwa Bize wakishawishi watu wampigie kura Davido...Amedai hata siku moja hakuwahi kumposti  kwa page zake kumpa sapoti hivyo asijadai leo kulia lia....

‘’Nikasikia kuwa kasema kuwa ndiyo maana wanaogopa kusapoti wasanii wa Tanzania kwa sababu wakisapoti wanadhalilishwa yeye mpaka naenda kuchukua tuzo ya Mtumbuizaji Bora yeye amenisapoti nini hajawahi kunipost hata tuzo moja sasa hivi ndiyo anajishaua eti ananipa hongera kwa tuzo ningemuona wa maana angepost watu wapige kura na kuwahamasisha ili ushindi urudi nyumbani lakini kwa chuki alizojazwa pasipo na sababu na roho mbaya aliyowekwa na watu imemfanya ashindwe kunipost na kutengeneza chiki za chinichini wakidhani wakiwapigia kura Wanageria mimi nitakosa tuzo Mungu amewalaani mimi nimeshinda halafu anajifanya anatoa hongera eti wanasapoti muziki wa Tanzania au kwasababu wameona tuzo imekuja ndiyo wanajifanya wanatoa hongera tuache unafiki,’’alimalizia Diamond.

0 comments:

Post a Comment