Pages

Subscribe:

Friday, July 31, 2015

NE-YO AELEZA KWANINI ALIKUWA NA HAMU YA KUONANA NA DIAMOND

Muimbaji wa Marekani, Shaffer Chimere Smith maarufu kama Ne-Yo ameitaja sababu iliyomfanya atake sana kukutana na Diamond Platnumz. “Baada ya watu kusikia kuwa nilikuwa nakuja kwenye MAMAs jina pekee ambalo walikuwa wakilitaja kwangu ni Diamond Platnumz,” Ne-Yo alimwambia Vanessa Mdee kwenye interview ya MTV Base.
“Nikasema ni lazima nikutane na huyu jamaa, nahitaji kumuona,” aliongeza.
Siku moja kabla ya tuzo hizo pia... Diamond alielezea jinsi Ne-Yo alivyomtafuta. “Wakati nazungumza na D’banj @salaam_sk alinifata na kuniambia @neyo anakutafuta anataka kukuona…” Ungependa kujua kilichofata??? Kaa karibu na TV, Radio yaani Kiufupi Media zako Soon utayaskia,” aliandika Diamond kwenye Instagram.

Ne-Yo na Diamond ni miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye MTV MAMA 2015.

0 comments:

Post a Comment