Pages

Subscribe:

Sunday, July 19, 2015

WEMA AMWANGUKIA KAJALA NA KUTAKA WAMALIZE BEEF

Msanii wa filamu nchini na Mkurugenzi wa Endless Fame Production, Wema Sepetu, amedai kuwa yupo tayari kumaliza bifu lake na msanii mwenzake Kajala Masanja, baada ya kutokuwa katika maelewano mazuri kwa muda mrefu. Bifu hilo lilichukua sura mpya ambapo Wema, alikataa kabisa kumsamehe mwanadada Kajala, na kujiapiza kuwa kamwe hawezi kumsamehe licha ya Kajala kutaka kumaliza tofauti hizo.
Wema amesema kuwa hakuna mwanadamu asiye na mapungufu na kumtaka Kajala  kuonana naye na kumaliza tofauti zao kwani... nafsi yake imeshamsamehe na imemuongoza kufanya hivyo.

Amedai kuwa kila jambo lina mwisho wake, hivyo amekaa chini na kufikia uamuzi huo ambao anaamini kabisa hapa duniani hakuna mtu asiyekuwa na moyo wa huruma na kusema kuwa hana budi kuyapuuza yaliyopita.



Amesema kuwa hana tatizo na Kajala, na kutaka watu kuamini kuwa amejitolea kumaliza tofauti hizo na kudai kuwa yupo radhi kukutana naye sehemu yoyote kuongea ili wale wasiomuamini wapate kuamini.

Kwa upande wa Kajala, amedai kuwa anashukuru kusikia hivyo na kudai kuwa hana tatizo na mtu na kumshukuru Wema, kwa uamuzi wake kwani alijitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha kuwa wanamaliza tofauti zao kwa njia mbalimbali lakini alikataa.

“Nimekuwa nikipigania hilo kila kukicha, sasa naamini Mungu atakuwa amesikia kilio changu kwa mara nyingine, napenda kusema sina tatizo lolote katika hilo,” alisema Kajala.

0 comments:

Post a Comment