Pages

Subscribe:

Thursday, July 16, 2015

IZZO BIZNESS: SIWEZI TENA KUIMBA SIASA




Izzo Bizness ni msanii kutoka Tanzania aliyetamba na nyimbo ya Ridhiwan ambayo alifanya vizuri na ilimtambulisha vyema katika mzuki wa Tanzania, Izzo Bizness ameeleza kuwa hawezi kuimba tena Siasa kwa sababu Ridhiwan... imebeba vitu vingi sana.
Akizungumza kwenye 255 ya XXL Izzo Bizness amesema "Siwezi kuimba Politics kwa sababu Ridhiwan imebeba vitu vingi hata nikiimba Politics ntarudia vitu asilimia nyingi ambavyo nimeimba kwenye Ridhiwan, kutokana na ukubwa wa ile nyimbo na heshima kubwa ya ile nyimbo nahisi inabidi nitulize akili hata nikija na Politics nakuja katika angle ambayo kweli watu watasema asante kwa sababu ukiachana na Ridhwan imeleta neno kama ongea na mshua, wazee wamebadilishwa siku hizi majina wanaitwa wakina mshua majina ya zamani, ngoma yenyewe kwa ujumla mambo ambayo tumeongelea mule ndani ni mambo ambayo yatadumu hata kama atakuja Rais ana jina lingine lakini ujumbe ambao alipewa Rais kwenye ule wimbo ulimfikia Rais hata kama atakuja Rais mwingine...Nimeona nichill coz hata yale ambayo nimeyaongelea kwenye Ridhwan bado hayajafanyiwa kazi."

0 comments:

Post a Comment