Pages

Subscribe:

Tuesday, March 22, 2016

JAYDEE: NILILALA NIMEAMKA TENA


ladyjaydee
Unapozungumzia wakongwe wa Muziki wa Bongo Fleva kwa upande wa wanawake, jina la Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ hutaacha kulitaja miongoni mwao. Kwa zaidi ya miaka 15, mkongwe huyu ameweza kukaa kwenye muziki pasipo kutete-reka huku kila baada ya kipindi akiibuka na nyimbo ambazo zinakuwa gumzo.
 
Tangu mwaka 2000 hadi sasa ameshanyakua tuzo zaidi ya 25 za ndani na nje ya nchi huku akishiriki katika tuzo zaidi 10 zikiwemo Afrimma, Kora, Kisima pamoja na Kili.
Jide ambaye...
hufahamika kwa majina tofauti kama vile Komando, Anakonda, na Binti Machozi baada ya kuachia albamu sita ambazo ni Machozi, Binti, Moto, Shukrani, Best of Lady Jaydee, Nothing But the Truth sasa ameamka tena na kuachia albamu yake ya saba ya Naamka Tena.

Katika makala haya anafungukia machache kuhusiana na ujio wake mpya;

Over The Weekend: Kwa nini umetumia jina la Naamka Tena?
Jaydee: Ujue katika maisha nimepitia changamoto nyingi sana, ukianza tangu nipo kwenye gemu ya muziki huu nimekuwa nikipitia changamoto, nalala na kuamka tena hivyo hata ujio wangu huu umetokana na misukosuko ambayo nimeipitia hususan kwenye ndoa na sehemu nyingine ndiyo maana nikasema Naamka Tena.


Over The Weekend: Ujio wako huu mpya (Wimbo wa Ndi Ndi Ndi) una video yake? Jaydee: Hapana, nimeanza kwanza kwa kutoa audio kisha baada ya hapo nadhani ni wiki mbili kutoka sasa natarajia kutengeneza video hivyo mashabiki wajiandae kumuona Jide kivingine.

Over The Weekend: Wimbo wa Ndi Ndi Ndi umeupika wapi?
Jaydee: Wimbo nimeutunga mwenyewe kwa kushirikiana na Terence Mwakaliku lakini umepikwa Studio za Rockstar4000 chini ya Prodyuza Naava Grey wa nchini Uganda.

Over The Weekend: Tutegemee nini baada ya ujio huo? Jaydee: Ni albamu yangu ya saba nitakayoingiza sokoni na baada ya hapo nitawataarifu mashabiki wangu kitakachofuata.

0 comments:

Post a Comment