Pages

Subscribe:

Wednesday, March 9, 2016

BAJETI NI KITU MUHIMU KWENYE MOVIE

Lulu


Mshindi wa filamu bora Afrika Mashariki kwenye tuzo za African Magic Viewers Choice 2016, Elizabeth Michael aka Lulu, amesema bajeti ni muhimu kwenye filamu.



Lulu ambaye ametua jana mchana akitokea nchini Nigeria zilipofanyika sherehe za tuzo hizo na kupokewa na watu wengi wakiwemo mastaa wa filamu, watu maarufu pamoja na mashabiki wa movie. 


Akizungumza na 255 ya XXL inayoruka kupitia Clouds FM, Lulu amesema, “Kitu muhimu cha kuzingatia kwenye filamu zetu ni...
bajeti, ukiangalia movie za wenzetu zilizoshindanishwa zinaonekana kuwa na bajeti nzuri.”


“Huu ni wakati kwa wadau mbalimbali kuwekeza kwenye filamu zetu nawahakikishia itawalipa sana, lakini pia inaweza ikawa ni biashara nzuri Zaidi kuliko biashara nyingine,” aliongezea Lulu.

0 comments:

Post a Comment