Pages

Subscribe:

Thursday, March 24, 2016

HARMONIZE KUITOA FAMILIA YAKE KIJIJINI KUILETA JIJINI DAR

Harmonize: Nafanya mpango kuitoa familia yangu kijijini kuileta Dar
Harmonize anang’ara kwa sasa lakini safari yake hadi kufika hapo alipo leo imekuwa ngumu na yenye misukosuko mingi. Ni msanii aliyetoka kwenye maisha duni katika kijiji chao kilichopo wilayani...

Tandahimba, Mtwara kwenye familia kubwa yenye wake wengi wa baba yake ambaye ni sheikh.

Kwa mama yake, walizaliwa watoto watatu huku yeye akiwa mtoto wa pili kuzaliwa.
Baba yake ana wake wengine watatu na watoto wengine takriban wanane lakini aliachana na mama yake akiwa bado mtoto hivyo amekulia kwenye familia yenye mama tu. “Mimi nimezaliwa bush kweli, hata umeme hatuujui. Mimi nimekuja town mwaka 2009 tu,” anasema. Hiyo ni baada ya kushindwa kuendelea na sekondari baada kuishia kidato cha tatu kutokana na baba yake kupendelea zaidi mwanae asome elimu ya akhera (elimu ya dini ya kiislamu)

Dar alifikia kwa dada yake ambako baada ya muda ajikuta akipishana na shemeji yake na kuamua kuanza kuishi mwenyewe kwa kufanya kila kibarua kilichojitokeza mbele yake. Kuna wakati hadi alikuwa akilala kwenye stendi ya basi ya mikoani iliyopo Temeke.

Wakati huu ambao maisha yamebadilika baada ya kusaini na WCB, Harmonize hajaisahau familia yake na ana mipango mikubwa. “Ninafanya mpango familia yangu nije niishi nayo vizuri hapa kwasababu kijijini kwetu kuna mazingira magumu sana sidhani kama mtoto mwenye akili timamu unaweza ukafurahia aishi maisha ya tabu wakati wewe unaishi maisha mazuri,” anasema. “Nilikuwa nafanya mpango panapo majaaliwa nilikuwa naongea na management yangu ili kuwa comfortable zaidi basi ikiwezekana hata familia yangu isogee hapa.” #Regrann

0 comments:

Post a Comment