Pages

Subscribe:

Friday, March 11, 2016

HAYA NDIYO MAJIBU YA DNA BAADA YA DIAMOND KUPIMA NA TIFFAH

Hii ni EXCLUSIVE stori! Kufuatia kelele kibao kutoka kwa wadau mbalimbali kwamba mtoto wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, yaani Latifah ‘Tiffah’ aliyemzaa na Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ si wa nyota huyo, hatimaye, jamaa ameamua kupima vinasaba ‘DNA’ (DeoxyriboNucleic Acid).

ISHU ILIKUWA AFRIKA KUSINI
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, Diamond aliamua kutekeleza mpango huo nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ ambako aliamini hakuna... ‘macho mengi’ ya watu, hususan mapaparazi.

SIKIA HII
“Jamani mimi nataka niwape stori ambayo ni ya uhakika. Hivi mnajua kwamba Diamond aliamua kwenda Sauzi kupima DNA yake na mtoto wake Tiffah?
“Kutokana na manenomaneno ya watu, ilifika mahali alichoka, akawa njia panda. Hivyo ili kuondoa figisufigisu, akamwambia Zari waende wakampime DNA mtoto na yeye. Ni kabla hajaenda Marekani.”

MAJIBU HAYA HAPA
Chanzo hicho kikasema: “Majibu ya DNA yamesema, Nasibu Abdul ni biological father (baba wa damu) wa mtoto Tiffah. Ilibidi jamaa amwage chozi maana alifikiria mengi, watu wamesema sana kuhusu yeye na Tiffah, kwamba si mwanaye, mara ni mtoto wa Ivan (Ssemwanga, mtalaka wa Zari), mara ni mtoto wa pedeshee mmoja wa Bongo. Yaani mengimengi yalisemwa.”

0 comments:

Post a Comment