Pages

Subscribe:

Saturday, March 26, 2016

IVAN AJIBU MAPIGO KWA DIAMOND NAYE AIPELEKA FAMILIA YAKE IBIZA

Inaitwa clash of the titans na siri ya mchezo hapa ni fedha ndiyo inayoongea na sio maneno matupu! Diamond na Zari wapo Ulaya kwenye vekesheni inayoendana na ziara ya From Tandale to The World, na sasa ex wa Zari, Ivan ameamua kujibu mapigo kwa kuipeleka familia yake (watoto aliozaa na Zari), kula bata... Ibiza.
Yeye anasema, “Flying out to Ibiza just to get some pizza …..#holidayGoals #squadGoals.” Seems like competition kati ya Ivan na Zarimond haiwezi kuisha leo wala kesho.

Kwa taarifa yako tu ni kwamba Ibiza ni kisiwa kilichopo kwenye bahari ya Mediterranean, kilomita 150 kutoka pwani ya mji wa Valencia, mashariki mwa Hispania. Ibiza ni kisiwa cha maraha kinachofahamika kwa maisha ya usiku na muziki wa house.

0 comments:

Post a Comment