Pages

Subscribe:

Wednesday, February 21, 2018

PENZI LA FID Q NA KARMA CHANZO CHADAIWA KUWA NI KITABU

Mpenzi wa msanii Fid Q anayejullikana kwa jina la Karima, ameweka wazi kitu kilichowakutanisha wawili hao, ambacho wengi hawawezi kuamini kwa ulimwengu wa sasa. 

Wakizungumza msichana huyo ambaye ni Mtanzania lakini huishi Uingereza, amesema kitu kilichowakutanisha wawili hao ni kitabu ambacho alitakiwa...
amkabidhi Fid Q alipokuja Tanzania.

“Nilikuwa nakuja Tanzania, kuna mtu akanipa kitabu nije kumletea Fid Q, nikaja nikampigia simu lakini hakutokea, ikafika siku kulikuwa na show akaniomba niende nikaenda, na ndipo tukakutana, kwa wakati huo wote nilikuwa simjui Fid Q na wala sijui kama ni msanii mkubwa hapa bongo, basi nikampa kitabu chake kila mmoja akaishia zake”, amesema Karima.

Akiendelea kusimulia safari ya mahusiano yao, Karima alisema wakiwa wanaendelea kuwasiliana kama watu tu wanaofahamiana, ndipo masuala mengine yakaibuka ikiwemo kuja kumpikia pilau akirudi Tanzania kwani alikuwa haamini kama anaweza kupika chakula cha kitanzania kwa kuwa amekuaa sana Ulaya, na kuwa mwanzo wa wawili hao kuwa karibu na hatimaye kuwa wapenzi.

Fid Q ni miongonni mwa wasanii wachache ambao hawaweki wazi masuala ya maisha binafsi hususani mahusiano, lakini imekuwa kinyume kwa binti huyo kwani amekuwa akimpost mara kwa mara kwenye mitandao wakiwa wawili, huku akiweka jumbe tamu za mapenzi.

0 comments:

Post a Comment