Pages

Subscribe:

Wednesday, February 28, 2018

LINAH AWEKA WAZI IDADI YA WANAUME ALIOTEMBEANAO MPAKA KUOLEWA

Msanii Linah Sanga ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake wa 'Same boy' akiwa ameshirikiana na msanii Recho amefunguka na kuweka wazi idadi ya wanaume ambao ametembea nao na kufaidi penzi lake.  

Linah Sanga akiwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV amesema kuwa toka amekuwa Linah na watu kumtambua kama msanii ametoka jumla ya wanaume...
watano japo anadai kuwa kuna wanaume wengine ambao ametoka nao kimapenzi hawakumbuki.

"Kwa haraka haraka nishatoka kimapenzi na wanaume kama watano hivi toka watu wamenifahamu kama Linah, sina idadi kubwa sana japo siwezi kuwakumbuka wote wengine nimeshawasahau kabisa, kuna watu wana idadi kubwa ya watu wametembea nao sema tu ni kwa sababu si wasaniii" alisema Linah Sanga 

0 comments:

Post a Comment