Baada
ya muda mrefu kutoonekana pamoja, hatimaye msanii Young Killer ameweka
wazi kilichotokea kati yake na aliyekuwa mpenzi wake ‘Miss Hip Hop’.
Rapper huyo anayetamba na ngoma ‘Toto Tundu’ ameiambia Clouds Fm kuwa ni kipindi cha miezi sita sasa tangu waachane. “Kulikuwa na... kutoelewana kidogo hatuko pamoja sasa hivi kama miezi sita,” amesema Young Killer.
Hata hivyo ameongeza kuwa si usaliti uliopelekea kuvunjika kwa mahusiano
yao kwani hicho ni kitu cha kawaida bali kilichowaachanisha ni sababu
za ndani zaidi.
Mwaka 2016 Young Killer alitangaza kumuoa mrembo huyo aliyempa jina la
Miss Hip Hip na kila mara wote walipenda kujiachia katika mitandao ya
kijamii ila sasa ndio hivyo kila mmoja na maisha yake.
0 comments:
Post a Comment