Pages

Subscribe:

Tuesday, February 27, 2018

MTOTO WA TATU WA KIM KARDASHIAN AWEKWA HADHARANI

Leo February 27,2018 kupitia mtandao wa instagram, Staa Kim Kardashian ambaye umaarufu wake umekuja zaidi katika kipindi cha “Kardashians” huko nchini Marekani ambapo ameamua kuweka wazi uso wa mtoto wake wa tatu kwa mara ya kwanza katika mitandao ya kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Kim Kardashian ameandika “Baby Chicago”
Mtoto wa tatu wa Kim Kardashian na rapper Kanye West ambaye ni Chicago alizaliwa mwezi uliopita kwa njia...
ya upandikizaji “surrogate” ambapo mwanamke huyo alilipwa hela kwaajili ya kumzalia Kim Kardashian pamoja na Kanye West mtoto wa tatu.
 


Wazo hilo la upandikizaji lilikuja katika familia ya West ambapo Kim Kardashian alishindwa kubeba ujauzito kutokana na sababu za kiafya ambazo zingempelekea kupoteza maisha na hii ni kutokana na report aliyoitoa daktari wa Kim Kardshian.

0 comments:

Post a Comment