Pages

Subscribe:

Friday, February 23, 2018

NAY WA MITEGO AIZUNGUMZIA COMMENT YA GODZILLA KWENYE POST YAKE YA INSTA

Rapa Nay wa Mitego mwenye 'hit song' ya 'Mikono Juu' amefunguka na kumchana Godzilla kuwa yeye hawaimbii wasanii wenzake kama anavyofikilia bali anajua nini mashabiki zake wanachokihitaji.
 
Nay ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo 'PB' inayorushwa na East Africa Radio baada ya msanii mwenzake Godzilla kuwa wa kwanza kutoikubali wimbo wa mikono juu na kudai ni mbaya na...
vitu vingine vingi. 

"Mimi nimechukulia kama ni mtazamo wake tu japo siwaimbii wasanii wenzangu, najua watu wangu wanahitaji kitu gani na ndio maana tukienda katika 'show' huwa nakuwa mshindi wa kwanza kwa sababu nawajua mashabiki zangu. Siwezi kununa wala 'kum-maindi' Godzilla kwa kauli yake", amesema Nay

Kwa upande mwingine, Nay wa Mitego amesema mwaka huu 2018 amekuja na mwendo wa kupiga kazi ili kuweza kuufikisha mbali muziki wake.

0 comments:

Post a Comment