Pages

Subscribe:

Wednesday, February 28, 2018

USAIN BOLT ATAJWA KUPIGA KABUMBU OLD TRAFFORD MWEZI JUNI MWAKA HUU

Hii ni Good News kwa mashabiki wa Bingwa wa Olimpiki Duniani Usain Bolt hatimaye atapata nafasi ya kuchezea soka katika uwanja wa Manchester United wa Old Trafford.

Bolt atakuwa nahodha wa timu ya pamoja ya watu maarufu na wanasoka ambayo itashiriki mechi ya Soccer Aid ambayo itaandaliwa na Shirika la...
Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto (UNICEF) June 10.

Bolt amenukuliwa akisema “Ni ndoto yangu kufanikiwa kama mchezaji wa soka la kulipwa. kucheza dhidi ya baadhi ya wachezaji nyota, hilo litakuwa jambo la kufurahisha sana,” .

Manchester United wameandika kwenye ukurasa wao Facebook: “Inafanyika hatimaye … Usain Bolt ataonyesha ustadi wake katika kucheza soka katika uwanja wa Old Trafford  #SoccerAid!

0 comments:

Post a Comment