Inawezekana wewe ni moja kati ya wengi ambao hawajawahi kusikia ugonjwa wa kutokwa Machozi ya Damu, Wataalamu wanasema kuwa kupitia uchunguzi walioufanya wamegundua kuwa ugonjwa huu unatokana na...
kasoro kwenye vinasaba (genes) za binadamu jambo ambalo hupelekea matatizo kwenye mishipa ya damu na hatimaye damu kuvuja maeneo ya mwili kama machoni.
Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha London katika Taasisi ya Afya ya Watoto na Hospitali ya Great Ormond Street (GOSH), ambao walishiriki utafiti huo, wameeleza kuwa kupatikana kwa ugunduzi huo kutasaidia kupatikana tiba ya ugonjwa huo.
Haya yametokea baada ya kesi mbalimbali za watu kuwa na ugonjwa huo maeneo mbalimbali duniani.
0 comments:
Post a Comment