Pages

Subscribe:

Wednesday, February 28, 2018

MTO NILE WAMFANYA MSANI MAARUFU NCHINI MISRI KUTUPWA JELA

Mwimbaji wa Misri Sherine Abdel Wahab amehukumiwa miezi sita gerezani kwa kutania juu ya hali ya usafi wa mto Nile.

Sherine, ni mmoja wa waimbaji maarufu nchini humo pia ni jaji katika kipindi cha mashindano ya waimbaji, The Voice- alimwambia mashabiki wake kuwa kunywa maji kutoka mto huo kunaweza kumpatia...
vijidudu. “Kunywa Evian badala yake.” alitania mwimbaji huyo. 

Bi Amer – ambaye hana umaarufu kama Sherine – alipatwa na hatia ya ‘kuchochea ufitini na uovu”. 

Sherine, amehukumiwa na mahakama moja Cairo kwa kusambaza habari zisizo za kweli. 

Chombo cha habari Misri, Ahram kimesema aliagizwa kulipa paundi 5,000 za Misri.
Mwimbaji mwingine, Laila Amer, pia alihukumiwa siku ya Jummane kifungo cha miaka miwili kutokana na video ya muziki.

0 comments:

Post a Comment