Haya ni matatizo ya kila siku na wanawake wengi ni swala linalotukumba wengi wetu.Wengine hadi kufikia kuficha sehem hizi za mwili sababu zinawa aibisha au...
wanaona aibu kuzionyesha .
Kama na wewe ni muhanga basi nakupa
baadhi ya tips tena home remedies ambazo zinatoka jikoni kwako ili
kukusaidia kufanya ngozi hizi za sehem mbili kuna na unafuu na kumaliza
tatizo.
Kwanza tujue kwamba matatizo haya ya ngozi kua rough na nyeusi kwenye magoti na viwiko vya mikono inasababishwa na nini???
1.sehemu hizi zinaukosefu wa glands za mafuta kitu kinachopelekea ziwe kavu haraka na hadi kua nyeusi kuliko kawaida.
2.Mara nyingi wengi wetu hizi sehem huwa
wala hatuzijali ,tunaziacha zenyewe unakuta ile layer ya ngozi iliyokufa
haiondolewi inakaa tu na kufanya pawe pagumu na pakavu.
3.Kingine mkusanyiko wa dead cells kwenye
sehem hizi kunasababisha kuwe rough na ile layer inatakiwa kuwa
inaondolewa mara kwa mara ili ku renew ile ngozi.
Cha kufanya basi ili kutoa huo ugumu na weusi wa magoti na viwiko vya mikono
1.Scrub ya sukari
Scrub inasaidia kupeel/kuondoa cells
zilizokufa ambazo zinasaidia cell mpya kutengenezwa na kufanya ngozi
kuonekana nzuri na soft.
Kutengeneza scrub hii unahitaji
Changanya Kijiko kimoja cha Asali na
sukari ya kawaida ,pakaa/sugulia kwenye goti lako au viwiko vya mikono
kwa mwendo wa duara ,Ile sukari itasaidia kutoa ile ngozi ambayo
haitakiwi,then osha na maji safi ,unatakiwa kufanya hizi kwa wiki mara
moja.
2.Limao na juice ya viazi ulaya
Viazi ulaya na limao zina properties za bleach which inazifanya ziwe chaguo la wengi kwenye mambo ya urembo
Mahitaji
Kata limao nusu sugulia kwenye
elbows/knees au kata pia kipande cha kiazi mviringo na ufanya the same
kama limao ,hii itasaidia kufanya ngozi hii iwe lighter .Then tumia
Asali ambayo itasaidia ku moisturize ngozi yako pia.
3.Oil massage
Mafuta yanaingia kwenye ngozi na kusaidia
ku moisturize naturally na internallu ,sababu hizi sehem hazina oil
glands kwa kuzi masage na mafuta mara kwa mara na olive ,almond au
coconut oil/mafuta ya nazi,kutasaidia pia pa shine ,So massage na mafuta
moja wapo kati ya hapo na acha usioshe mafuta yaingie vyema kwenye
ngozi.
4.Tumia dodoki au Jiwe lile laini
ukioga waweza tumia jiwe laini au dodoki
kusugua sehem za magori na viwiko vya mikono,usisugue kwa nguvu just be
gentle ,itasaidia ku exfoliate ngozi ayako ,si lazima kufanya kila siku
unaweza pata vidonda na ukiwa unasugua fanya kwa circular motion.
5.Moisturiser
Chukua mafuta yako paka kwenye ngozi ili
kusaidia paendelee kua soft ,baada ya hizo remedies zote ukishafanya
hakikisha huachi magoti yako na elbow bila kupaka mafuta hii itasaidia
pasiwe pakavu na rough.
0 comments:
Post a Comment