Pages

Subscribe:

Friday, February 23, 2018

MCHUMBA WA MO MUSIC AOLEWA NA NA MTU MWINGINE BAADA YA MO KULIPA MAHARI

mo
Msanii wa Bongo fleva Moshi katemi jina lakisanii Mo Music, anaetamba na wimbo wake wa Bajaji, amejikuta akiwa kwenye msongo wa mawazo baada ya mwanamke aliye kusudia kumuoa aitwaye Iptisam kuolewa na mtu mwengine.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo karibu na msanii huyo, Mo Music alikuwa ameshatoa posa hadi mahari lakini tatizo likawa kwenye...
dini; yeye Mkristo binti Muislam na wote hawakuridhia kutoka kwenye dini zao, ndipo msichana huyo akachumbiwa na mtu wa dini yake na kuamua kumtosa mshkaji bila kurudisha mahari.

Kutokana na ishu hiyo paparazi wetu alimvutia waya Mo Music ambaye alikuwa na haya ya kusema; “Dah umenitonesha kidonda, ni kweli demu kaolewa wiki iliyopita, kitendo cha kubadili dini ningewakera wazazi wangu ndo’maana nikawa nasuasua, tupo kwenye mvutano waturudishie mahari yetu wanatuzungusha.”

0 comments:

Post a Comment