Pages

Subscribe:

Monday, February 26, 2018

WIZKID ATAMANI KUFUNGA NDOA KTK FUKWE ZA TANZANIA

Tanzania inaaminika kuwa ni moja kati ya nchi za Afrika zenye vivutio vya utalii, moja kati ya tweet zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kwa sasa ni pamoja na hii ya staa wa muziki wa Nigeria Wizkid kudaiwa kuandika katika twitter account yake kuwa anatamani ndoa yake afunge akiwa Tanzania.

Tweet hiyo imesambaa katika mitandao ya kijamii na wengi kujiuliza ni kweli Wizkid anatamani kufunga ndoa Tanzania nini...
kimemvutia? “Natamani kufunga ndoa katika beach za Tanzania”

Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa Wizkid kusifia beach za Tanzania, miezi kadhaa iliyopita akifanya interview akiwa nje ya Tanzania alitaja kuwa katika nchi alizotembea Afrika na kufurahia  Tanzania ni moja wapo hususani beach(fukwe) za Tanzania

0 comments:

Post a Comment