Pages

Subscribe:

Monday, February 26, 2018

ROSA REE AFUNGUKA NAMNA ANAVYO SHAWISHIWA NA KHALIGRAPH JONES

Rosa Ree Afunguka Kuhusu Mahaba Yake kwa Khaligraph Jones 
Msanii wa muziki Bongo, Rosa Ree amefunguka jinsi anavyovutiwa na uwezo wa kimuziki wa rapper kutoka nchini Kenya, Khaligraph Jones.
Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa amekuwa karibu na Khaligraph Jones kutokana anamshawishi... kufanya vitu vikubwa katika muziki wake.
“Khaligraph Jones is also brother of mind, ni mtu ambaye nina ukaribu sana naye, pia yeye anani-inspire sana kutokana na issue zake ambazo anazifanya,” amesema.
“Ni mpambanaji sana, hustler sana atahakikisha anafikia lile lengo ambalo analo na ni kitu ambacho kinani-inspire mimi kama female rapper, Kaligraph pia ni mtu ambaye ana moyo wa pekee yake,” ameongeza.
Mwaka jana Rosa Ree alimshirikisha Khaligraph Jones katika remix ya ngoma yake inayokwenda kwa jina la One Time. Rosa Ree kwa sasa anatamba na ngoma ‘Marathon’ aliyomshirikisha Bill Nass.

0 comments:

Post a Comment