
Kisa cha mwanafunzi mmoja wa chuo
kikuu nchini Tanzania kuuwawa kwa risasi wakati polisi ya nchi hiyo
ilipokuwa ikitawanya kile walichokiita mkutano usio halali wa wafuasi wa
upinzani kimeibua maswali na hisia kali miongoni mwa umma juu ya
kiwango cha nguvu ambacho polisi hutumia wanapokabiliano na
waandamanaji.
uchunguzi bado unaendelea kubaini aliyehusika na kifo hicho.
Lakini Tanzania haiko peke yake. Aghalabu idara za polisi katika nchi nyingi za Afrika zimejipata lawamani katika mikasa mingi ya aina hiyo kwa kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa kudhibiti fujo na ghasia ikiwemo matumizi ya silaha za moto ambazo taathira zake huwa kifo au majeraha ya kudumu kwa aliyelengwa.

Hali ikoje barani Afrika?
Ingawa
suala la polisi kulenga raia kwa silaha za moto ni la kilimwengu
ukipigia mfano wa matukio kama hayo nchini Marekani dhidi ya raia weusi,
hali ni dhaifu zaidi kwenye nchi maskini na zaidi Afrika ambapo ni
nadra makosa kama hayo kuripotiwa au wakosaji kushughulikiwa kisheria.Karibu watu 122 waliuliwa na polisi katika matukio mbalimbali kati ya mwaka 2016 hadi mwanzoni mwa 2017.
Maelezo ya taarifa hiyo yalifichua kwa jumla ukweli kwamba polisi katika nchi za Afrika ikiwemo Afrika mashariki hutumia nguvu kupita kiasi na huenda mbali zaidi ya kanuni za mifumo ya ulinzi iliyoboreshwa na jumuiya ya kimataifa zinazoweka kikomo cha matumizi ya nguvu na hasa silaha za moto dhidi ya raia.
Polisi wanaweza kutumia silaha za moto?
Umoja wa Mataifa kupitia afisi yake ya masuala ya ulinzi wa Haki za Binadamu umeweka masharti katika azimio la Havana la mwaka 1990 la Matumizi ya Nguvu na silaha za moto kwa wasimamizi wa sheria.
'Iwapo polisi italazimika kutawanya mikusanyiko batili ambayo haina rapsha wala vurugu wanapaswa kujiepusha kutumia nguvu. Pindi italazimu nguvu kutumika basi iwe ya kiwango cha chini kadiri iwezekanavyo' inasema sehemu ya ibara hizo.
Hata hivyo malalamiko makubwa ya watu ni kuwa masharti hayo ambayo yameorodheshwa pia kwenye sheria nyingi za nchi za afrika yamekuwa yakipuuzwa, na mara kadhaa polisi imeonekana kupendelea zaidi njia za kikatili za kutumia silaha za moto hata kama mikusanyiko na maandamano ni tulivu.
Polisi wanafunzwa nini vyuoni?

Lakini kuna wasiwasi iwapo maafisa wa polisi wanazingatia mafunzo haya.
Maafisa wa polisi wana mafunzo ya kutosha?
Mauaji
ya raia 34 kwenye mgodi wa Marikana nchini Afrika Kusini yaliyofanywa
na polisi kwa kutumia bunduki za rashasha yaliongeza miito ya kuitaka
serikali ya nchi hiyo kulifanyia marekebisho jeshi la polisi la nchi
hiyo ambayo limekuwa na rekodi mbaya katika udhibiti wa ghasia kwa
kutumia silaha za moto. Taarifa hizo ziliibua swali kubwa, ikiwa Afrika Kusini, moja ya nchi zilizopiga hatua muhimu za maendeleo hasa ya uchumi barani Afrika, ina tatizo la aina hiyo yumkini hali ni mbaya zaidi kwa nchi nyingine ambazo hutenga bajeti ndogo ya mafunzo ziada kwa maafisa wa polisi na wala hazitoi ithibati ya kukabidhiwa na kutumia silaha za moto.
Kuna njia mbadala?
Mataifa yaliyoendela yanatumia njia kadhaa zinazokubalika kitaalamu kuwa haziwezi kuleta madhara makubwa au majeraha ya kudumu kwa mlengwa. Gesi za kutoa machozi, maji ya kuwasha, risasi za mpira na hata virungu vya plastiki vinaweza kusaidia.
Siyo kwamba vifaa na mafunzo ya kutumia mifumo haipo Afrika, laa! Ni vile tu polisi wa Afrika inazingatia nguvu na mabavu kuwa suluhu la kila jambo kwenye usimamizi wa sharia.
Polisi inaweza kubadilika Afrika
Kwa
jumla itachukua muda kwa idara za polisi barani Afrika kubadilika kwa
sababu nyingi hufanya kazi kwa shinikizo za viongozi wa siasa na
watawala ambao ndiyo watoa amri wakuu kwa vyombo hivyo vya usalama. Utambuzi huo utasaidia kuzifanya idara za polisi zilenge zaidi kutoa huduma badala ya mabavu na watawala kujielekeza kwenye kutimiza ahadi za kampeni na Maisha bora ya watu badala ya kuwekeza mamilioni ya fedha kununua silaha au kugharamia mazishi ya raia wasio na hatia waliouwawa kwa risasi.
0 comments:
Post a Comment