Pages

Subscribe:

Friday, February 23, 2018

FA KUMPA ADHABU GUARDIOLA BAADA YA KUUNGA MKONO MAANDAMANO YA CATALAN



Kocha wa Club ya Man City ya England Pep Guardiola amejikuta akiingia matatizoni na chama cha mpira cha England FA, baada ya kuonekana akisapoti jimbo la Catalonia la nchini Hispania kudai uhuru wake kuwa kama nchi uhuru.

Pep Guardiola ni miongoni mwa wahispaniola wanaounga mkono jimboa la Catalonia kujitenga na Hispania na kupata uhuru kama nchi lakini baada ya kuonekana Pep Guardiola katika baadhi ya mechi zake ameonekana akivaa...
riboni ya kusapoti Catalonia kupata uhuru wake amezua utata.

Baada ya kuonekana hivyo chama cha soka England FA kimetangaza kutaka kumuadhibu Pep Guardiola kwa kuonekana akifanya movement za kisiasa katika soka za kudaiwa kusapoti kudai uhuru wa Catalonia katika game za soka zinazosimamiwa na FA.

Pep ambaye kikosi chake cha Man City kinajiandaa na game ya fainali ya Carabao Cup dhidi ya Arsenal watakayocheza Jumapili ya February 25 2018, amepewa muda na FA hadi Jumatatu saa 20:00 kutolea ufafanuzi uvaaji wake wa ribon hiyo ambayo ameonekana nayo pia katika press conference ya kuelekea game ya fainali ya Carabao Cup.

0 comments:

Post a Comment