Pages

Subscribe:

Monday, December 14, 2015

HII NDIYO SCENE ILIYO MLIZA DIAMOND KWENYE WIMBO WA UTANIPENDA

12224632_1624698111126002_1129176434_n


Diamond Platnumz aliamua kuitumia familia nzima kwenye video ya wimbo wake mpya, Utanipenda!
Mchumba wake Zari, mwanae Tiffah, mama yake Sandra na mameneja wake Babu Tale na Said Fella wameonekana. Hata hivyo scene ya mama yake inayomuonesha akienda kwa Jakaya Kikwete na kufukuzwa na pia kwa Said Fella na kufukuzwa pia ilimliza Diamond.
 
“Wakati hii scene inashutiwa sikuweza kabisa kukaa karibu, ijapokuwa ilikuwa ni uigizaji ila nikajikuta najiskia vibaya alivyokuwa anafukuzwa na kuendelea...
kubembeleza. Hata siku ya kwanza kuiona hii video mara ya kwanza na pili machozi yalinitoka,” ameandika Diamond kwenye Instagram.

“Pia ilichukua muda sana kuizoea hicho kipande maana ilikuwa kila nikijikaza na kuchkulia ni maigizo ila najikuta mood inabadilika. Ooh mama yangu ntakulipa mimi.”
Video hiyo hadi sasa ina views zaidi ya laki tatu tangu iwekwe Ijumaa iliyopita.

0 comments:

Post a Comment