Pages

Subscribe:

Thursday, December 17, 2015

MWANA FA KUTOA VIDEO MBILI (SAFI NA CHAFU) ZA WIMBO WA AHSANTENI KWA KUJA



FA
Baada ya Mwana FA kuachia wimbo wake mpya ‘Asanteni Kwa Kuja’ wiki hii, amesema kuwa video ya wimbo huo iliyoshutiwa Afrika Kusini ina version mbili (Dirty & clean), safi ikiwa ni kwaajili ya TV za nyumbani na chafu kwaajili ya TV za nje.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, FA amesema maamuzi ya kufanya version mbili yalikuja baada ya kuwa na...
mabishano kati yake na director wa video hiyo kuhusu kipi kitoke na kipi kibaki.

Amesema baada ya kutumiwa video aliona kuna vipande vingi ambavyo visingefaa kuonyeshwa kwenye runinga za hapa nyumbani, hivyo alitaka sehemu hizo ziondolewe huku director wake akikataa kuziondoa.

“Video ilivyokuja nikamwambia hii video ilivyo local chanel za hapa kwetu haiwezi kuonyeshwa, ikabidi nimwambie sekunde hii mpaka hii utoe, jamaa akabisha kabisa akasema hiyo ndiyo video yenyewe, kwa hiyo atachoweza kufanya ataziondoa zile parts ambazo mimi nimesema, lakini huku ambako ana uhakika video inacheza jinsi ilivyo ataipeleka kama ilivyo, haikuwa lengo langu kutengeneza video mbili ila mazingira yalinipeleka huko,” alisema Mwana FA.
Mwana FA aliongeza kuwa hakufahamu moja kwa moja kama director alipanga kufanya video ya namna ile.

“Mi nililetewa script lakini haikuwa na details moja kwa moja kwamba watu watakuwa wamevaa nini, wata act vipi, mi mwenyewe ilibidi nisafiri na begi mbili kuhakikisha nina kila kitu ninachokitaka, ulipofika muda ndo nikaona wamevaa hivi, wanakuwa directed wafanye hivi,” alisema Mwana FA.

0 comments:

Post a Comment