Pages

Subscribe:

Thursday, December 17, 2015

JUX AKWAMA KUMALIZIA MJENGO WAKE

Maponda


Mkali wa ‘One More Night’ Jux ameeleza sababu ya kukwama kuendelea kwa ujenzi wa mjengo wake wa kifahari ambao miezi kadhaa aliuonesha kwenye mitandao ya kijamii.
Muimbaji huyo amedai kuwa kwa sasa amesimama kidogo kuendeleza mjengo wake na kuwekeza pesa katika kufanya...
muziki ikiwa ni pamoja na kuendelea kufanya video zenye ubora.

“Unajua kwa sasa kidogo nimesimama kuendeleza nyumba hivyo, ipo siku watu watakuja kuona mjengo ukiwa umekamilika maana maisha yetu sisi wasanii hayawezi kufichika. Nimesimama sababu pesa ninazopata nimezielekeza katika kufanya muziki na video kali,” alisema Jux.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo alieleza jinsi anavyoweza kufanya video kali zinazomgharimu pesa nyingi wakati haonekani akifanya show nyingi kama wasanii wengine.

“Ni kweli hata Jumatatu (jana) nitaondoka na kurudi shule nchini China, lakini kwa sasa ninachofanya ni kuwekeza katika muziki huku nikiamini baadaye hiki ninachofanya sasa kitanilipa. Hivyo najenga ukaribu na mashabiki wangu na Mungu akijalia nikamaliza masomo yangu nchini China nitaanza kufanya show za uhakika. Unakuta hata sasa hivi natafutwa sana ili nifanye show lakini bahati mbaya huwa nakuwa nje ya nchi na kuzikosa show hizo,” alifafanua.
 

0 comments:

Post a Comment