Pages

Subscribe:

Thursday, December 31, 2015

HUYU NDIYE MISS WA KWANZA TANZANIA ALIYE TWAA TAJI MWAKA 1967

Mwaka 1960 ndipo Mashindano ya urembo nchini yalipoanza na hayatakuwa na
muonekano wa kimataifa kwa sababu yalifanyika kwenye maeneo machache.
Kwani kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kwamba mrembo wa kwanza kunyakua
taji hilo la Miss Tanzania, si mwingine bali alikuwa Theresa Shayo.


Kutokana na maadali na utamaduni ya mtanzania serikali ililazimika
kuyapiga marufuku mashindano hayo ilipofika tu mwaka 1967, kabla ya Rais
wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuyaruhusu kuendelea kutokana
na...

utandawazi kuanza kushika kasi ya ajabu.

Tangu kipindi hicho nchi yetu ya tanzania iliweza kufanikiwa kutoa
warembo kadhaa walioshiriki mashindano ya kumtafuta mrembo wa dunia,
wakiwemo Emil Adolf, Nancy Sumary, Saida Kessy, Basila Mwanukuzi, Hoyce
Temu, Jacqueline Ntuyabaliwe na wengineo.


Mshindi huyo wa kwanza kushiriki mashindano hayo ya urembo ya Miss
Tanzania Theresa Shayo, alifariki dunia huko Augburg Munich Ujerumani na
kuzikwa uko uko alikokuwa akiishi miaka yote hiyo.


Mwaka 1967 ndipo hayati Theresa alitwaa taji hilo kwenye shindano
lilofanyika hoteli ya Kilimanjaro, alifariki dunia january 26 mwaka 2007
na maradhi ya kansa ya tumbo huku akiwa na umri wa miaka 61.


Theresa hakubahatika kupata mtoto na alikuwa akiishi mjini Augsburg
ambako aliolewa na mjerumani aitwaye Chrstian Rieger ambaye waliachana
na hadi anakufa alikuwa akiishi na boy friend aitwaye Tonny.


Kabla ya hapo Theresa alikuwa akiishi peke yake mtaa wa Schmiedberg
namba 9 katikati ya mji wa Augsburg na alimwachia nyumba hiyo mtanzania
aitwaye Othman Lukindo.


Kwani alikuwa ni mtu mwenye huruma sana pamoja na kwamba alijiengemeza
zaidi kwa ndugu zetu wa Kenya, alikuwa na upendo na kila mmoja uko
alikokuwa akiishi alimpenda.

Miss Zanzibar wa kwanza Hediye Khamis Mussa (kati)
akiwa na washindi wa pili na watatu January 13, 1968
 Mashindano
haya yamekuwa yakitia fora na kujizolea umaarufu mkubwa ndani ya jamii
ya watanzania, hasa baada ya kuwa chini ya uratibu wa Hashim Lundega,
ambaye alianza kuyaendesha tangu mwaka 1994.

Kwani kupitia Lundega, kampuni mbalimbali zimekuwa zikijitokeza
kudhamini mashindano hayo na kutoa zawadi zikiwemo za magari ya kisasa
kwa washindi, hali iliyoyafanya yawe na ushindani mkali.

Ukuaji wa Mashindano haya ulikuwa ni wa kasi kubwa kwani watu wengi kama
ilivyo kwa mchezo wa soka ama muziki, hasa baada ya muziki wa
kitanzania kuingiliwa na vionjo vya kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo).

Mkoa wa Mbeya nao haupo nyuma katika mashindano hayo.
Umekuwa unapita katika hatua hizo kwa kupata warembo mbalimbali
walioibuka washindi kuanzia ngazi ya mkoa, kanda hadi kufikia hatua ya
kushiriki shindano la ‘Miss Tanzania’.

0 comments:

Post a Comment