Pages

Subscribe:

Tuesday, December 29, 2015

HANSCANA AKWAMISHA WIMBO MPYA WA TEMBA KUTOKA

Temba


Temba amedai kuwa Hanscana ndiye aliyesababisha kuharibika kwa ratiba yake ya kuachia video ya wimbo wake mpya, Fundi.


Rapa huyo ambaye miezi michache iliyopita aliwaahidi mashabiki wake kuachia wimbo ‘Fundi’ aliyowashirikisha Yamoto Band na Jokate, ameimbia Bongo5 kuwa kazi hiyo haitoweza kutoka tena mwaka huu. “Nimeshindwa kutoa ngoma kwa sababu nilipanga kutoa audio na video lakini director Hanscana akawa...
amesafiri South Africa kwa short project, lakini akakaa mwezi mmoja na nusu ndio maana nikashindwa kutoa project kwa sababu nilihitaji kutoa video na audio,” amesema Temba.
Pia rapa huyo amesema sababu nyingine ya kukwama kwa project hiyo ni kuingiliana kwa ratiba na Chege.

“Kitu kingine Chege wakati anaenda Afrika Kusini na mimi nilitakiwa kwenda lakini nilishindwa kutokana na passport yangu iliisha muda. So nikaona bora nisupport kazi ya Chege halafu mwakani ndio ya kwangu itoke.”

0 comments:

Post a Comment