Pages

Subscribe:

Saturday, December 19, 2015

IZZO AWAJIBU MASHABIKI WALIO IPONDA VIDEO YA SHEM LAKE

Msanii Izzo Bizness amewajibu mashabiki wake na kutoa maelezo ya kutosha, kuhusu kwa nini video yake inaonekana haina ubora tofauti na walivyotarajia, ingawa yeye ameridhishwa na video hiyo.
 
Izzo B ameyasema hayo Jana, baada ya kupata tuhuma kuwa mashabiki wameiponda video hiyo. “Kutengeneza story au script ile kazi nilimuachia Khalfan, na video tumefanyia Kigamboni kwa hiyo kuna baadhi ya characters ambao ilibidi...
wawepo ichezeke ile stori, kabisa ilishindikana yani pale ni namna ambavyo yeye alijitahidi, na sioni kama kuna ubaya wowote”, alisema Izzo Bizness.

Izzo Bizness aliendelea kwa kusema kuwa video hiya inafanya vizuri kwani toka aiachie haijafikisha masaa 24 lakini tayari video hiyo imeshatazamwa na watu zaidi ya elfu 8.

“Mpaka sasa hivi tunaongea hatujafikisha masaa 24 bado na zaidi ya watu 800 ambao wameshaangalia mpaka sasa hivi mitandaoni, kwa hiyo ni dalili nzuri kabisa na asilimia 90 ya comments zimekuwa positive”, alisema Izzo Bizness.

Kwa upande wake Director Khalfan ambaye ndiye alitengeneza na kuongoza video hiyo, amesema kwake yeye haoni ajabu kwa kazi zake kukosolewa, na kwamba watu wafahamu kuwa video ya muziki ina utofauti na video za movie.

“Hilo suala kwanza sasa hivi kama nimelizoea hivi kwa sababu mara ya kwanza ndio lilikuwa linanipa chalenge sana, ilishawahi kunitokea kwenye video ya Ben Pol, lakini sioni sababu ya kusema hawajaelewa, music video sio movie kwamba kile kitachoimbwa kionekane”, alisema Khalfan

0 comments:

Post a Comment