Pages

Subscribe:

Monday, December 14, 2015

MR BLUE AWEKEZA PESA ZAKE KWENYE VIDEO HII MPYA

blue


Mr Blue Kabayser ana video nyingi alizowahi kufanya lakini amekiri kuwa video mpya ‘Baki Nami’ ndio ya kwanza kuwekeza pesa yake mwenyewe.

Blue amesema kuwa kazi zote zilizopita amekuwa akifanya kwa ‘kuunga unga’ na kusaidiwa na washikaji zake bila yeye kutoa chochote, kitu ambacho kilisababisha...
asiwe anapata kazi bora. 

Ameongeza kuwa ‘Baki na Mimi’ ndiyo video iliyomsumbua kukamilisha visa vyote alivyoviimba, sehemu ya gharama ikiwa ni kukodisha limousine yenye gharama ya shilingi milioni 1 kwa siku, gauni la zaidi ya shilingi laki 4 na vitu vingine vingi ambavyo amevilipia mpaka kazi nzima ili kuwasilisha kazi nzuri kwa mashabiki.

Blue amesema kuwa, kazi hii inavunja utaratibu wake wa awali wa kuendesha sanaa yake kwa ubahili kidogo, akiwa amejipanga sasa kwaajili ya kuwekeza pesa ili kupata pesa kutoka katika muziki.

0 comments:

Post a Comment