Pages

Subscribe:

Monday, December 14, 2015

JUX: KUFANYA MUZIKI KWA KUZINGATIA MAADILI NI KUJIKOSESHA FURSA



12317695_1056396384405644_446158107_n
Muimbaji wa muziki wa R&B aliyewahi kupata dhoruba la kufungiwa kwa video ya wimbo wake ‘Uzuri Wako’ na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kwa kigezo cha maadili, ameeleza jinsi kigezo hicho kinavyoathiri wasanii na kushindwa kupiga hatua.

Jux aliyeachia video ya wimbo wake mpya ‘One more Night’ hivi karibuni, amekiambia kipindi cha FNL kinachoruka kupitia EATV kuwa, kama wakiendelea kubanwa na kigezo hicho, wasanii wa Tanzania watashindwa kushindana na...
wasanii wa kimataifa.

“Unajua muziki wetu bado ni mchanga sana kwa hiyo tukisema kila kitu kiwepo kama tunavyotaka sisi Watanzania ni ngumu sana. Kwahiyo sometimes sisi kama wasanii tunaofanya muziki tukitaka tuendelee mbele, kama mtu unasema unataka kuwa international halafu unafanya kazi za kitanzania huwezi kwenda mbele,” alisema.

“Kwahiyo kama unataka kazi yako iwe international unatakiwa uamue kufanya kitu ambacho shabiki kitamvutia na kina uhalisia. Tunatoa pesa nyingi sana kwenye video, tunataka video zetu ziende mbali zaidi na watu ambao wanataka kuona wanataka kuona ni kitu gani ambacho unaimba na jinsi gani kinaendana na matendo ya video, kwahiyo ukisema tuweke utanzania, haina maadili haina nini hatuwezi kwenda popote. Kuna vitu ambavyo hatutakiwi kivipitiliza vya kawaida.”
Video zingine zilizowahi kufungiwa kupigwa kwenye TV kwa kigezo cha maadili ni ‘Sugua Gaga’ ya Shaa, ‘Kabinti Special’ ya Dully Sykes na zingine.
 

0 comments:

Post a Comment