Pages

Subscribe:

Thursday, December 17, 2015

OMMY DIMPOZ KUZINDUA ACHIA BODY SIKU HII HAPA

Inawezekana ni muda mrefu sana haujamsikia Ommy Dimpoz akizimiliki headlines kwenye ma Radio na TV, sasa time anatarajia kuachia single mpya iitwayo Achia Body iliyotayarishwa na Man Water & Mo Fire. Akiongea na ripota wa millardayo.com alisema:’Baada ya kimya cha muda mrefu kutokana na tours zangu kwahiyo imepita kipindi kirefu sana mashabiki zangu walikuwa wanasubiri ujio wangu ndio maana nikaona sio vibaya kuwapa zawadi ya... kufungia mwaka pamoja na sikukuu ya Chrismas’>>> Ommy Dimpoz
‘Ndio maana nimeamua kuachia rasmi hii single yangu iitwayo Achia Body imetayarishwa na Man Water & Mo Fire, video nimeshoot Afrika Kusini kikubwa tu zaidi watu wajiandae kucheza muziki mzuri kwahiyo ni ngoma ambayo itawapa watu furaha, na kesho ndio siku ambayo nitaizindua video ya single hiyo mpya pale AKEMI Golden Jubilee Town Dar es Salaam‘>>>Ommy Dimpoz

0 comments:

Post a Comment