Pages

Subscribe:

Tuesday, December 29, 2015

DIAMOND: SIKUKATA JINA LA NAHREEL KWENYE BEAT YA NANA

Diamond


Siku kadhaa zilizopita mtayarishaji wa muziki wa studio ya The Industry, Nahreel alilalamikia kitendo cha utambulisho wake ‘Nahreel on the beat’ kuondolewa kwenye hit song ya Diamond Platnumz ‘Nana’ ambayo ndiye aliyei-produce.


Diamond naye amepata nafasi ya kueleza sababu ya utambulisho huo kutokuwepo kwenye wimbo huo. Baba Tiffah amesema kuwa mwanzoni wakati anataka kushoot video hiyo Nahreel alimpa demo ambayo ilikuwa bado haijawekewa sign hiyo, hivyo baada ya...
kushoot na director kumaliza ku edit, alipopewa audio ambayo imekamilika ikawa imeongezwa sign, kitu ambacho kwa director ingempa kazi kutokana na kuongezeka kwa sekunde ambazo kwenye demo iliyotumika mwanzo hazikuwepo.


“so mara ya pili alivyonipa sasa video ilishaisha nataka iliyokuwa mastered akawa ndio ameweka sign” amesema Diamond kupitia 255 ya XXL. “Haikuweza kufit kwasababu ilikuwa inazidisha sekunde halafu ilikuwa inaanza mwanzo mara kumi ingekuwa mwisho…inamaana editor aanze kukatakata na kuedit tena upya kitua ambacho tulikuwa tumeshachelewa. Kwahiyo ilichelewa kuwekwa ingekuwa imewekwa kuanzia mwanzo ingekuwa rahisi lakini sina sababu ya kusema nimkate producer kwasababu kama producer kafanya kazi yake kubwa lazima apewe credit zake.” Alisema Diamond.

“Ile nyimbo imefanyiwa mastering na Tudd Thomas, mtu anaweza kusema labda Tudd Thomas ndo kaichekecha, sio kweli ilichelewa na sioni sababu ya kumfanya Mtanzania mwenzangu kutokumpa credit zake katika nyimbo aliyoitengeneza katumia jasho lake nitakuwa na roho mbaya sana. Director akasema nataka iwe kama ilivyokuwa mwanzo mkinipa nyingine haiwezi kufit, aah sasa ntafanyaje kitaalam mi sijui nikaona basi tukachukua ile ile ya mwanzo.” Alimaliza Diamond.

0 comments:

Post a Comment