Pages

Subscribe:

Saturday, December 19, 2015

COUNTRY BOY AKANUSHA KUWA NA BEEF NA YOUNG DEE

Mtu Chee


Rapa wa kundi la Mtu Chee, Country Boy amesema hana tatizo na Young Dee licha ya kupishana lugha miezi michache iliyopita baada ya rapa huyo kujitoa katika kundi hilo.

Country Boy anasema hajawahi kuoongea na Young Dee toka atangaze kuachana na Mtu Chee. “Sina tatizo na Young Dee, yeye alichagua...
kufanya kile anachokitaka na sisi tuliendelea na Mtu Chee,” ameiambia Bongo5.

“Ila bado ni mshikaji wangu, haya mambo hutokea kwenye muziki ingawa kuna watu nasikia wanasema mimi nina tatizo na BOB sio kweli. Mimi niko poa na kila mtu, hata Nyandu Tozi sina tatizo naye.” Kundi hilo ambalo limebaki na wasanii wawili, Country Boy na Stamina, linajiandaa kuachia kazi mpya, likimshirikisha rapa yoyote ili kukamilisha idadi ya rapa watatu.

0 comments:

Post a Comment